Psalms 87

Sifa Za Yerusalemu

Zaburi ya wana wa Kora. Wimbo.

1 aAmeuweka msingi wake katika mlima mtakatifu;
2 b Bwana anayapenda malango ya Sayuni
kuliko makao yote ya Yakobo.
3 cMambo matukufu yanasemwa juu yako,
ee mji wa Mungu:
4 d“Nitaweka kumbukumbu ya Rahabu
Rahabu hapa ni jina la ushairi la Misri.
na Babeli
miongoni mwa wale wanaonikubali mimi:
Ufilisti pia na Tiro, pamoja na Kushi,
Kushi hapa ina maana ya Naili ya juu, yaani Ethiopia.

nami nitasema, ‘Huyu alizaliwa Sayuni.’ ”

5 gKuhusu Sayuni itasemwa hivi,
“Huyu na yule walizaliwa humo,
naye Aliye Juu Sana mwenyewe
atamwimarisha.”
6 h Bwana ataandika katika orodha ya mataifa:
“Huyu alizaliwa Sayuni.”
7 iWatakapokuwa wanapiga vinanda wataimba,
“Chemchemi zangu zote ziko kwako.”
Copyright information for SwhNEN